Kudeki na kupuliza marasi katika haram tukufu na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Siku ya Jumatatu mwezi (14 Muharam 1443h) sawa na tarehe (23 Agosti 2021m), kazi ya kudeki, kupuliza marashi na kutandika mazulia imefanywa ndani ya haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yanayo izunguka, baada ya kumaliza ziara ya mwezi kumi Muharam pamoja na matembezi ya Towareji na kumbukumbu ya kuzikwa miili mitakatifu.

Kazi hiyo imefanywa na idara ya kusimamia haram tukufu na wahudumu wa kitengo cha utumishi na Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya mbele ya mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Dhiyaau-Dini na marais wa vitengo.

Sayyid Mustwafa Dhiyaau-Dini ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Jioni hii baada ya kumaliza maombolezo ya Ashura, tumefanya usafi na kupuliza marashi katika haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tumezowea kufanya hivi kila mwaka, tunapenda kufanya kazi usiku mwingi kwa sababu huwa hakuna watu wengi, jambo ambalo hutupa wepesi wa kudeki, muda mfupi kabla ya kuanza kazi tulisoma Ziaratu-Ashura na ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa pamoja, kama sehemu ya kuomba ruhusa ya kufanya kazi hiyo, mwisho tukiwa chini ya kubba takatifu tumeomba dua Mwenyezi Mungu awape afya na amani wananchi wa Iraq”.

Kiongozi wa Idara inayo simamia haram bwana Nizaar Ghani Khaliil amesema: “Kazi iliyofanywa ni usafishaji na upulizaji wa marashi kwa kuanzia katika dirisha takatifu, kwa kutumia vifaa maalum, kisha tukaelekea sehemu zinazo zunguka dirisha, hadi kwenye korido nne za eneo hilo, tumedeki na kuosha ukuta pamoja na kupuliza dawa, sambamba na kuondoa kila aina ya kitu kinacho weza kuharibu muonekano, baada ya kazi hiyo tumetandika upya miswala”.

Makamo rais wa kitengo cha uangalizi wa haram Ustadh Zainul-Aabidina Adnani amesema: “Shughuli ya usafi imefanywa katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kutandua miswala maalum iliyo tandikwa katika siku za maombolezo ya Ashura, na kuipeleka sehemu ya kuoshea mazulia ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambapo yameanza kuoshwa moja kwa moja, halafu tumetandika miswala mipya, na kurudisha mazingira ya Ataba katika hali ya kawaida kama ilivyokua kabla ya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: