Mafanikio ya mkakati wa kitengo cha Dini katika ziara ya mwezi kumi Muharam

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza, kufanikiwa kwa mkakati wake wa kitablighi na kitamaduni katika ziara ya mwezi kumi Muharam, wamenufaika mamia ya mazuwaru, maandalizi yanaendelea kwa ajili ya kumi la pili na ziara ya Arubaini.

Makamo rais wa kitengo hicho Shekh Aadil Wakiil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Huu ni mwaka wa pili ambao tunakua na utaratibu maaluma katika ziara ya Ashura kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, upande wa uhudhuriaji ulikua:

  • - Kufungua vituo vya kupokea mazuwaru na kutoa maelekezo na nasaha, na kujibu maswali yao.
  • - Kufanya vikao vya uombolezaji ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku zote kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam.
  • - Kuchangia katika uendeshaji wa majlisi za kuomboleza na kutoa mihadhara ya kidini ndani na nje ya Karbala.
  • - Kuratibu shughuli za uombolezaji kwenye miji tofauti mkoani Mosul.
  • - Kushiriki kupokea waombolezaji wa matembezi ya Towareji na wanaohuisha kumbukumbu ya kuzikwa miili mitakatifu ya mashahidi wa Karbala.
  • - Kushiriki katika vipindi tofauti vya luninga”.

Wakiil akabainisha kuwa: “Amma kuhusu upande wa kimtandao, tumerusha mafundisho mbalimbali kwenye mitandao ya mawasiliano ya kijamii na tulifungua link maalum ya kitengo cha Dini kwa ajili ya kujibu maswali na kutoa maelekezo, sambamba na kuweka namba za simu maalum kwa ajili ya kujibu maswali na kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali, tulikua tunafanya kazi zaidi ya saa (12) kwa siku”.

Akamaliza kwa kusema: “Baada ya kumaliza program iliyodumu kwa muda wa siku kumi za mwanzo katika mwezi wa Muharam, tumeanza kutekeleza mkakati wa siku kumi za pili, utakao fuatiwa na mkakati wa siku kumi za tatu, kisha tutaingia katika mkakati wa mwezi wa Safar kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: