Kukumbuka kuuawa kishahidi kwa Imamu Hussein (a.s) katika uwanja wa chuo kikuu cha Al-Ameed

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya maombolezo ya kuuawa kishahidi kwa Imamu Hussein (a.s) na harakati yake takatifu iliyolinda Dini tukufu ya kiislamu.

Shughuli hiyo imeandaliwa na kitengo cha maelekezo ya kinafsi na kimalezi katika chuo hicho, na kuhudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali, na marais wa baadhi ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya, pamoja na viongozi wa Dini na kisekula na viongozi wa chuo.

Shughuli ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na mmoja wa wanafunzi wa famasia katika chuo hicho, halafu yakasomwa mashairi kuhusu Imamu Hussein (a.s) na mwanafunzi kutoka kitivo cha famasia bwana Ahmadi Hassan Haidari, baada ya hapo akapanda kwenye mimbari Shekh Abdullahi Dujaili na akaongea kuhusu maisha, jihadi na kuuawa kishahidi kwa Abu Abdillahi Hussein (a.s) na familia yake takatifu, akahitimisha kwa kusoma tenzi za uombolezaji zilizo amsha hisia ya huzuni na majonzi kutokana na vita ya Twafu na kumkumbuka bibi Zainabu (a.s) namna alivyo shuhudia kuuawa kwa kaka yake, kisha kikagawiwa chakula cha kutabaruku na kumbukumbu ya familia ya Mtume (s.a.w.w).

Mkuu wa kitengo cha maelekezo ya kinafsi na malezi katika chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Hassanaini Mussawi amesema: “Kufanya majlisi za aina hii kunaimarisha uhusiano kati ya mtu na tukio la Imamu Hussein (a.s) pamoja na harakati yake, ni utambulisho wa ufuasi wa kweli, na nafasi nzuri ya kutambulisha vizavi kiigizo chema na watu sahihi wa kufatwa kutoka katika historia ya maisha ya familia ya Mtume (s.a.w.w)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: