Kiongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ametembelea kituo cha turathi za Najafu

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) ametembelea kituo cha turathi za Najafu kilicho chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Ataba tukufu.

Amepokewa na mkuu wa kituo hicho Ustadh Mhakiki Ahmadi Ali Alhilliy, ambaye ameeleza kazi za uhakiki zinazofanywa na kituo mbele ya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kazi zao zinaonyesha kasi ya ukuaji wa elimu.

Mheshimiwa Sayyid Swafi amesisitiza: “Umakini wa kazi na uhakiki wa taarifa za kielimu, sambamba na kufanya kazi zinazo acha athari nzuri katika sekta ya turathi, na kwamba lengo la kuanzisha kituo hiki ni kuthibitisha nafasi ya elimu katika mji wa Najafu, na kuonyesha nuru yake mbele ya miji mingine pamoja na miji hiyo kukosa mambo yaliyopo katika mji wa mlango wa elimu”.

Hii ni sehemu ya ziara anazofanya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu kila wakati, hutembelea vituo na taasisi za kielimu zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya, kwa ajili ya kuangalia utendaji wa kazi na kuhakikisha kazi inaendelea vizuri.

Tambua kuwa kituo cha turathi za Najafu, kinahusika na kuhakiki turathi za Najafu kisha kuziweka katika faharasi na kuzitangaza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: