Muwakilishi wa shirika la afya la kimataifa katika mkoa wa Karbala: Tunaimani na mazingira ya afya hapa mkoani

Maoni katika picha
Muwakilishi wa shirika la afya la kimataifa hapa mchini Iraq, Dokta Ahmadi Zawitan ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuangalia maandalizi ya ziara ya Arubaini katika sekta ya afya.

Muwakilishi wa shirika la afya la kimataifa hapa Iraq Dokta Ahmadi Zawitan katika ziara hiyo amesema: “Tumeridhika na mazingira ya afya katika mkoa wa Karbala, baada ya kuona kiwango kikubwa cha maandalizi yanayo fanywa na wizara ya afya na mkoa wa Karbala kwa kushirikiana na Ataba takatifu”, akaongeza kuwa: “Nimekuja Karbala kuangalia maandalizi yanayo fanywa kwa ajili ya ziara ya Arubaini ijayo, na kuangalia msaada unaoweza kutolewa na shirika la afya la kimataifa katika tukio hilo”.

Akabainisha kuwa: “Katika ziara ya Arubaini watu wanaweza kufika milioni (15), huo ni mkusanyiko mkubwa zaidi wa binaadamu katika uso wa dunia, tupo tayali kutoa ushirikiano wowote utakao hitajika na wizara ya afya, mkoa wa Karbala na Ataba takatifu, ili kupunguza hatari inayo weza kutokea kwa watu wengi kiasi hicho kukusanyika katika mji mmoja kwa wakati mmoja”.

Akasema kuwa: “Kuna kikao kitakacho fanyika hivi karibuni kujadili utekelezaji wa ziara ya Arubaini, ukizingatia kuwa: “Kuna mkutano mwingine wa kimataifa utafanywa mwanzoni mwa mwaka ujao chini ya shirika la afya hapa Iraq, utakaojadili mazingira ya ziara za kidini na mikusanyiko”.

Dokta Osama Abdulhassan kiongozi wa idara ya madaktari katika Atabatu Abbasiyya tukufu amesema: “Muwakilishi wa shirika la afya la kimataifa hapa Iraq Dokta Ahmadi amekagua maandalizi ya kiafya na njia za kujikinga na maambukizi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya, pamoja na kuangalia maandalizi maalum ya ziara ya Arubaini”.

Akaongeza kuwa: “Shirika la afya la kimataifa kupitia muwakilishi wake hapa Iraq kuja kuangalia maandalizi yanayo fanywa na Ataba tukufu katika sekta ya afya na kujikinga na maambukizi, kwa kuandaa hospitali na vituo vya afya, kunaonyesha ukubwa wa kazi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: