Kikosi cha Shamia kinatoa zawadi kwa mshindi wa shindano la (Qutufu) la kuhifadhi Qur’ani tukufu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imehitimisha shindano la (Qutufu) la Qur’ani, mahafidhi wengi wa Qur’ani wameshiriki kutoka mikoa tofauti ya Iraq, kikosi cha Shamia kimekua mshindi wa kwanza na kikosi cha Karbala mshindi wa pili.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu Shekh Jawadi Nasrawi amesema: “Katika kuendeleza kazi zinazofanywa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika kuhudumia vizito viwili, idara ya tahfiidh imefanya shindano la kuhifadhi Qur’ani kwa jina la (Qutufu), zaidi ya wanafunzi (24) kutoka mikoa tofauti ya Iraq wameshiriki, nao ni wanafunzi wa Maahadi na matawi yake ya mikoani”.

Akabainisha kuwa: “Washiriki wa shindano hili ni wale waliohifadhi juzu tano tu, walikua vikundi nane, vimeonyesha ushindani mkali”, akaongeza kuwa: “lilikua moja ya malengo ya Maahadi kuhakikisha wanashiriki katika shindano la kitaifa au kimataifa, miongoni mwa vipengene vya shindano hili ni kupima kipaji cha kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, ikiwa ni Pamoja na kutaja namba za aya na kurasa, na walisomewa maneno ya aya halafu mshiriki anakamilisha aya”, akasema: “tumefanya hivyo kupima vipaji vyao na kuwafanya watwalii zaidi walicho hifadhi”.

Akaendelea kusema: “Mwisho wa shindano hili tumetoa zawadi kwa kikosi kilichoshinda nafasi ya kwanza na ya pili, kwa lenge la kuwashajihisha waendelee na safari ya kuhifadhi”,

Tambua kuwa shindano limesimamiwa na idara ya tahfiidh katika Maahadi, lilikua na ushindani mkubwa katika kila hatua, ushindani huo uliendelea hadi hatua ya mwisho, chini ya jopo la majaji wafuatao (Ustadh Alaa-Dini Alhamiri hukumu za usomaji, Ustadh Hafidhu Hami ubora wa kuhifadhi na Haidari Jalukhani Mussawi sauti na naghma).

Kumbuka kuwa shindano lilirushwa na vituo vingi vya luninga, kikiwemo kituo cha luninga cha Al-Iraqiyya, na kituo cha Albalad, kupitia masafa ya bure iliyo tengenezwa na kituo cha wataalamu Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: