Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ametembelea chuo kikuu cha Al-Ameed kukagua maendeleo ya kielimu na kiujenzi katika chuo hicho.
Amepokewa na rais wa chuo hicho Dokta Muayyad Ghazali na wasaidizi wake pamoja na wakuu wa vitivo.
Amekagua mazingira ya kielimu kwa ujumla na kuangalia matokeo ya mitihani ya mwisho wa mwaka, pamoja na kukagua hatua ya mwisho ya ujenzi na kusikiliza maelezo kuhusu maendeleo ya kielimu na kiidara.
Mheshimiwa amepongeza kazi nzuri inayofanywa katika sekta ya elimu.
Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya kila kiwezalo katika kuendeleza sekta ya elimu, utamaduni na malezi hapa Iraq.