Kufungua mlango wa kushiriki katika program ya (Yanabii haamil Aljuud)

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeandaa program ya (Yanabii haamil Aljuud) kwa ajili ya watoto wenye umri wa miaka (5 – 11).

Kiongozi wa kituo hicho bibi Asmahani Ibrahim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Program hii inalenga kubaini vipaji vwa watoto mapema na kuviendeleza, tumeunda kamati ya kupokea washiriki itakayo wakusanya na kuwatahini”.

Akaongeza kuwa: “Tunaomba wazazi wahimize watoto wao kuja kushiriki kwenye program hii, na kuhakikisha wananufaika na kipindi cha likizo ya kiangazi”

Akabainisha kuwa: “Tutapokea kazi za washiriki chini ya mada maalum watakazo pewa, watashiriki kwa njia ya mtandao, aidha kutakuwa na zawadi kwa watakao endana na malengo ya program”.

Kumbuka kuwa kituo cha utamaduni wa familia kinapanua wigo wa harakati zake, ili kuyafikia makundi tofauti ya watu katika jamii, kinanjia nyingi za kuifikia jamii, ikiwemo njia hii iliyoandaliwa na watalamu wa makuzi rika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: