Mawakibu za Karbala na watu wake na mazuwaru wanahuisha siku ya saba tangu kuawa Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Watu wa Karbala kupitia maukibu na vikundi vyao vya Husseiniyya kama kawaida yao kila mwaka, jioni ya mwezi (17 Muharam), ambayo ilisadifu siku ya Alkhamisi (26 Agosti 2021m), waliadhimisha siku ya saba tangu kuawa Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake.

Matembezi ya waombolezaji yalianzia katika barabara ya Kibla ya malalo ya Imamu Hussein (a.s), kisha wakafanya majlisi ya kuomboleza katika haram yake takatifu, halafu wakaenda katika malalo ya mwezi wa familia na mbeba bendera ya Twafu Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, matembezi hayo yamefanywa kwa uratibu wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu.

Walipoingia katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakafanya majlisi ya kuomboleza iliyo khutubiwa na Shekh Bahaau Karbalai, mtoto wa marehemu Shekh Haadi Karbalai (r.a), aidha wamekumbukwa pia watumishi wa matembezi ya Husseiniyya na waimbaji wa kaswida na tenzi za Ashura, waliokua na mchango mkubwa katika kuhuisha tukio hilo.

Wakati wa matembezi ya maukibu hiyo ambayo wameshiriki mazuwaru wa malalo mbili takatifu, zimeimbwa kaswida na tenzi za kuomboleza zilizo amsha hisia ya huzuni na majonzi, huku mazingira yakienyesha kauli isemayo, kama hakuna aliyetembelea kaburi lako siku ya saba tangu kuuawa kwako katika mwaka wa (61h) ewe Abu Abdillahi Hussein, wala haukuwashiwa mishumaa na kumwagiwa maji kaburi lako, na kufanyiwa matam, leo sisi wapenzi wako na wafuasi wako, watu wa Karbala tunakuja kukupa pole na kumliwaza mama yako Zaharaa na babu yako Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa msiba huu, na kupoza moto wa msiba wako usiopoa milele na milele.

Tambua kuwa vita ya Twafu ni tukio kubwa kwa kila mtu, kukumbuka tukio hilo ni jambo muhimu kwa wafuasi wa Abu Abdillahi Hussein (a.s), kila mtu hujiandaa kuhuisha tukio hilo, kiroho, kiakili na kimwili, uhuishaji wa tukio hilo humfanya mtu kutumia kila njia katika kuonyesha hisia zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: