Ummu-Kulthum (a.s): Mmeua watu bora baada ya Mtume (s.a.w.w)

Maoni katika picha
Wanahistoria wameripoti kuwa msafara wa mateka wa Imamu Hussein (a.s) ulipofika katika mji wa Kufa, watu wa mji huo wakawa wanawapa watoto walio katika msafara huo, baadhi ya vitu kama tende, mkate na karanga, Ummu-Kulthum akawaambia: Enyi watu wa Kufa, hakika kwetu sisi kupokea sadaka ni haram, akaanza kuchukua vitu walivyo kua wamepokea watoto na kuvitupa.

Muslim Jaswaswi anasema: Huku watu wanalia kwa yaliyowakuta, kisha Ummu-Kulthum akawaambia: Nyamazeni enyi watu wa Kufa, wanaume zetu wametuua, na wanawake mnatulilia! Hakimu katiyetu ni Mwenyezi Mungu siku ya hukumu, Ummu-Kulthumu akawahutubia kwa sauti ya juu huku analia, akasema:

Enyi watu wa Kufa mmefanya jambo baya sana, kwa nini mmemgeuka Hussein na kumuua, mmepora mali zake na kuteka wanawake wake na kuwanyanyasa? Mmeangamia kabisa.

Mmeangamia, mnajua ubaya gani mliofanya? Mzigo gani mliobeba? Damu gani mliyomwaga? Heshima gani mliyovunja? Haki gani mliyokiuka? Mali gani mliyopora? Mmeua watu bora baada ya Mtume (s.a.w.w), imeondolewa huruma katika nyoyo zenu, tambueni kuwa kundi la Mwenyezi Mungu ndio lishindalo, na kundi la shetani ni lenye hasara.

Kisha akasema:

Mmemuua kaka yangu akiwa mwenye subira mmeangamia * mtalipwa moto mkali unaofoka.

Mmemwaga damu ya nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu * aliyoharamisha Mwenyezi Mungu kisha Muhammad.

Tambueni makazi yenu kesho ni motoni * moto mkali wenye muwako mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: