Zaidi ya watu laki moja na elfu ishirini na tatu wamefanyiwa ziara ya Ashura kwa niaba

Maoni katika picha
Idara ya taaluma na mitandao chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imesema kuwa jumla ya watu (123099) wamefanyiwa ziara ya Ashura kwa niaba katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), waliojisajili katika mtandao wa Alkafeel (mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu).

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir, amesema: “Ziara ya mwezi kumi Muharam ni miongoni mwa ziara muhimu na inaratiba maalum, ambayo husimamiwa na masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu, walianza tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam, ambayo ni kufanya ziara, kuswali na kusoma dua”.

Akabainisha kuwa: “Maombi ya kufanyiwa ziara kwa niaba yamepokewa kupitia mitandao ifuatayo (Kiarabu, Kiengereza, Kifarsi, Kituruki, Kiurdu, Kifaransa, Kiswahili, Kijerumani), mitandao hiyo imepokea maombi mengi kutokana na mazingira ya sasa duniani na Iraq kwa Ujumla, yanayo pelekea idadi kubwa ya watu kushindwa kuja kufanya ziara”.

Akafafanua kuwa: “Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya waliongoza kufanya ziara hiyo tukufu ndani ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kufanya ziara ya mwezi kumi Muharam, wameswali na kusoma dua”.

Akamaliza kwa kusema kuwa: “Watu wengi waliojisajili wametoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistan, Urusi, Marekani, Uengereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuwait, Malezia, Australia, Aljeria, Bahrain, Misri, Ujerumani, Island, Namsa, Yunani, Holandi, Tunisia, Denmak, Norwey, Qatar, Aljeria, Ubelgiji, Moroko, Afghanistan, Oman, Ekwado, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Gana, Yemen, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijani, Qabrus, Finland, China, Ailend, Honkon, Japani, Imaraat, Sudani)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: