(Mtazamo wa Imamu Hussein -a.s- wa Qur’ani katika maisha) ndio mada ya nadwa ya Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Majmaa Ilmul-Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya nadwa chini ya anuani isemayo: (Mtazamo wa Imamu Hussein -a.s- wa Qur’ani katika Maisha), iliyo wasilishwa na Mheshimiwa Sayyid Rashidi Husseini, mmoja wa walimu wa hauza katika mji wa Najafu.

Nadwa imefanywa ndani ya Husseiniyya ya Abraar, imehudhuriwa na kundi kubwa la waumini na wadau wa Qur’ani, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyo somwa na Yusufu Fatalawi, baada yake Sayyid Husseini akaanza kuwasilisha mada yake, akaanza kwa kuelezea dunia katika mtazamo wa Qur’ani, na jinsi Imamu Hussein (a.s) alivyo ichukulia, na umuhimu wa kujihadhari nayo.

Akataja baadhi ya aya zinazo elezea dunia, sambamba na kufafanua aya zinazo kemea chuki, uadui na kila aina ya shari, akasoma aya, hadithi, riwaya na ushahidi wa kijamii, pamoja na kueleza mazingira ya kuuawa Imamu Hussein (a.s) -kama moja ya mifano ya wazi inayo onyesha kilele cha mtu kupenda dunia kwa waovu wa zama zile akiwemo Yazidi-.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya, hufanya nadwa kila mwezi hapa wilayani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: