Maahadi ya Qur’ani tukufu imeshiriki kwenye matembezi ya Husseiniyya ya mwaka wa tatu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, imeshiriki kwenye matembezi ya Husseiniyya ya mwaka wa tatu, yanayo simamiwa na muungano wa vikundi vya usomaji wa Qur’ani hapa Iraq kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Matembezi yameanzia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapita katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu hadi kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s), zaidi ya mikoa (13) ya Iraq imeshiriki katika matembezi hayo huku wakisoma tenzi kuhusu bwana wa mashahidi (a.s).

Wakahitimisha matembezi hayo kwa kikao cha usomaji wa Qur’ani kilicho fanyika ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s).

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni kituo muhimu cha fani za Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kutoa elimu ya Qur’ani na kutengeneza jamii yenye uwelewa wa Qur’ani katika kila sekta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: