Semina za Qur’ani zinaendeshwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa Ilmul-Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendesha semina nane za Qur’ani kwa wasichana wenye umri tofauti, katika makao makuu ya Maahadi yaliyopo Najafu na matawi yake yaliyopo mikoani, wanafundisha hukumu za usomaji na kuhifadhi chini ya wakufunzi mahiri wenye uzowefu mkubwa katika fani za Qur’ani.

Kiongozi wa Maahadi Bibi Manara Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tunaendesha semina nane kwa lengo la kuhusisha idadi kubwa ya watu watakao fikiwa na nuru ya kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, masomo yamepangwa kulingana na umri wa washiriki pamoja na ngazi zao kimasomo (sekondari, diploma na chuo), semina za kuhifadhi ni maalum kwa kundi la Baraaim, wanahifadhi juzu la thelathini”.

Akaongeza kuwa: “Semina hizi ni muendelezo wa harakati za Maahadi katika sekta ya elimu, zinalenga kueneza elimu ya Qur’ani kwa wanawake, washiriki wamewekwa makundi makundi kulingana na umri wao pamoja na viwango vya elimu zao, wakufunzi wanauzowefu mkubwa katika sekta hiyo”.

Akasisitiza kuwa: “Tumekusudia kufikisha elimu ya Qur’ani kwa idadi kubwa ya watu, hivyo imetubidi tutumie njia ya mtandao (elimu masafa) sambamba na njia ya mahudhurio inayofanywa katika ofisi za Maahadi zilizopo Najafu na matawi yake”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake hufanya harakati tofauti za Qur’ani kila mwaka zikiwemo semina za Qur’ani tukufu, lakini kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa, mwaka huu tumetosheka na harakati chache ikiwemo hii ya kutumia njia ya mitandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: