Kumaliza kuweka mapambo katika dirisha la bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitakatifu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wamemaliza kutengeneza sehemu ya mapambo yanayoitwa (Kalwi), yaliyopo katikati ya maandishi ya Qur’ani na mashairi, sehemu ya juu ya dirisha la kaburi la bibi Zainabu (a.s), sehemu zote nne zimetengenezwa kwa umaridadi mkubwa unaozidi dirisha la zamani.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo Sayyid Nadhim Ghurabi, akaongeza: “Hakika usanifu wa michoro ya mapambo ni muhimu katika dirisha, kazi hiyo hufanywa kwa mikono chini ya wachoraji wenye ujuzi mkubwa wa kuyayusha madini na kuyachonga, wataalamu wetu wamefanikiwa kukamilisha kazi hii kutokana na uzowefu walionao, mapambo hayo yatatiwa dhahabu baada ya kukamilika kama ilivyo katika mchoro”.

Akafafanua kuwa: “Pambo linavipande (14) kila kimoja kinauzito wa (kilo 2) na urefu wa (sm 128) na kimo cha (sm 32), vimetengenezwa kwa madini ya silva katika umbo la herufi ya (S) yenye ukubwa wa (ml 1), urefu wake kwa jumla unafika mita (16.78) vimezunguka dirisha pande zote, vimenakishiwa kwa mkono, sehemu ya mapambo hayo yapo kwenye dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na nyingine kwenye dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s)”.

Akaendelea kusema: “Kila sehemu ya pambo hilo (Kalwi) imepitia hatua nyingi, kuna hatua ya nakshi, hatua ya kuyayushwa kwa moto na hatua ya kusafishwa kwa kutumia vifaa maalum hadi hatua ya mwisho, kazi zote zinanfanywa kwa mikono, baada ya kumaliza kazi hiyo inafuata kazi ya kurekebisha shoo ya mbele, nayo inahatua mbalimbali pia, hadi kufikia hatua ya kutia dhahabu na kuwekwa kwenye umbo la dirisha la mbao, hapo ndio vinaunganishwa na sehemu ya chini na kuwa kitu kimoja”.

Akamaliza kwa kusema: “Sehemu hii sawa na sehemu zingine zilizo ongezwa katika dirisha, ni njia ya kitaalamu na kisasa inayotumika katika utengenezaji wa madirisha, sehemu zote zinaunganika vizuri na kuwa kitu kimoja, madirisha yote yaliyotengenezwa katika kiwanda hiki hutengenezwa kwa kufuata utaratibu huo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: