Atabatu Abbasiyya imechukua jukumu la kubeba wanafunzi 1300 wanaoenda kufanya mtihani wa wizara na chuo kikuu cha Al-Ameed kinawapa hifadhi..

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefungua vituo (12) vya kufanyia mitihani wanafunzi (1300) wanaohitimu masomo, kwa ajili ya kufanya mitihani ya mwisho iliyo anza kabla ya siku chache chini ya usimamizi wa idara ya malezi ya mkoa wa Karbala, kitengo kinatumia magari ya Atabatu Abbasiyya kubeba wanafunzi, kuwatoa majumbani mwao hadi kwenye vituo vya mitihani na kuwarudisha.

Makamo rais wa chuo katika mambo ya utawala Dokta Alaa Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni moja ya kazi za Atabatu Abbasiyya tukufu katika kusaidia watoto wetu wanafunzi wa ngazi tofauti, kutokana na kuwepo kwa changamoto ya maambukizi ya virusi vya Korona na kuongezeka kwa joto, chuo kimefungua milango ya kupokea wanafunzi wa darasa la sita kwa ajili ya kufanya mitihani ndani ya kumbi za chuo katika vituo (12)”.

Akaongeza kuwa: “Kulikua na maandalizi maalum yaliyofanywa kwa ajili ya mitihani, kuanzia maandalizi ya sekta ya afya na kujikinga na maambukizi sambamba na mpangilio wa wanafunzi kulingana na vituo vyao, pamoja na kuweka vifaa vyote vinavyo hitajiwa na wanafunzi katika mitihani, kama vile maji ya kunywa, viyoyozi, taa na mengineyo, ikiwa ni pamoja na kuandaa mazingira mazuri ya wasimamizi wa mitihani”.

Rais wa kitengo cha usafiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abduljawaad amesema: “Katika mkakati wa kubeba wanafunzi kuwatoa majumbani mwao hadi katika vituo vya mitihani na kuwarudisha, tumeandaa magari yenye ukubwa tofauti, kwa ajili ya kazi hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: