Mkuu wa idara ya usalama wa taifa ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mkuu wa idara ya usalama wa taifa la Iraq Ustadh Abdulghani Ajiil Asadi, ametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) leo siku ya Jumapili (20 Muharam 1443h) sawa na tarehe (29 Agosti 2021m) baada ya Adhuhuri.

Baada ya kufanya ibada ya ziara na dua amekutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqari katika ukumbi wa utawala, kwenye kikao hicho wamehudhuria pia wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.

Baada ya makaribisho wakajadili mambo tofauti, ikiwa ni pamoja na huduma ambazo Atabatu Abbasiyya inatoa kwa watu wanaokuja kutembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na huduma walizo toa hivi karibuni katika ziara ya mwezi kumi Muharam, katika mazingira magumu ambayo taifa linapitia, akafafanua kuwa Atabatu Abbasiyya imejiandaa kupokea mazuwaru wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kwa kuweka mazingira wezeshi ya kufanya ziara hiyo.

Mwisho Mheshimiwa mkuu wa idara ya usalama akapongeza kazi zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kisha wageni wakaaga na kuondoka kwa bashasha kama walivyo karibishwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: