Msikiti wa Hannanah.. sehemu kilipowekwa kichwa cha Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Msafara wa mateka wa familia ya Mtume (s.a.w.w), wakati ukiwa njiani kutoka Karbala kwenda Kufa kisha kutoka Kufa kwenda Damaskas Sham ulisimama sehemu nyingi, miongoni mwa sehemu hizo ni Msikiti wa Hannanah, msafara wa mateka ulipokaribia mji wa Kufa usiku wa mwezi kumi na mbili Muharam, walikaa hapo bila kuingia mjini, kwani Ubaidullah bun Ziyadi alitaka waingie mjini wakiwa pamoja na wanajeshi waliobeba siraha kwa nderemo na vifijo.

Msikiti wa Hannanah upo upande wa kaskazini mashariki ya Najafu kushoto mwa mtu anaekwenda Kufa, msikiti huo ulijengwa katika eneo kilipo wekwa kichwa cha Imamu Hussein (a.s) kabla ya msafara wa mateka kuingia katika mji wa Kufa.

Kwa mujibu wa wanahistoria wanasema kuwa “Hannanh” ni neno linalotokana na Hunain, msafara wa mateka wa Imamu Hussein (a.s) ulipopita sehemu ya Thawiyyah (muinuko upo karibu na muinuko unaoitwa Hannanah, kunamakaburi ya wafuasi wa kiongozi wa waumini (a.s), likiwemo kaburi la swahaba mtukufu Kumail bun Ziyadi -r.a-) walipofika hapo wakachezea kichwa chake na vichwa vya wafuasi wake.

Zikasikika sauti kutoka muinuko wa Hunain zikilalamika kwa wanavyo fanyiwa, neno hilo ni la kiarabu maana ya huruma, kwani limetokana na neno “Hanna” sehemu hiyo pakajengwa msikiti, kadri miaka inavyo kwenda yakatokea mabadiliko ya jina, kutoka “Hanna” hadi “Hannanah”. Ukajengwa msikiti huo na Mundhirul-Awwal bun Nu’maan wa kwanza, aliyetawala mwaka 418 – 462h, ilikua sehemu tukufu wakati wake.

Mufiid na Sayyid ibun Twausi na Shahiid wa kwanza katika mlango wa ziara ya kiongozi wa waumini (a.s) wanasema: Ukifika Alam -Hannanah- swali rakaa mbili. Imepokewa na Muhammad bun Abu Umair kutoka kwa Mufdhil bun Omari anasema: Imamu Swadiq (a.s) alipita sehemu hiyo akaswali rakaa mbili, akaulizwa: swala gani hiyo? Akasema: sehemu hii kiliwekwa kichwa cha babu yangu Hussein bun Ali (a.s), walikiweka hapa walipotoka Karbala, kisha wakakibeba hadi kwa Ubaidullah bun Ziyaad.

Msikiti wa Hannanah ni miongoni mwa misikiti mitukufu sana, watu hutabaruku hapo, na hutembelewa na majirani wa sehemu hiyo na mazuwaru, ni moja ya sehemu tatu alizoswali Imamu Jafari Swadiq (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: