Sahani laki tatu za chakula zimetolewa na mgahawa wa Atabatu Abbasiyya kwa mazuwaru wa Ashura

Maoni katika picha
Kitengo cha mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa kiligawa sahazi (300,000) za chakula kwa mazuwaru wa Ashura, kuanzia siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam hadi siku ya mwezi kumi na tatu, siku ya kumbukumbu ya kuzikwa muili wa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na wafuasi wake (r.a), huduma ya kugawa chakula imezingatia kanuni za afya, kuanzia uandaaji, upishi hadi ugawaji, kulinda usalama wa mazuwaru na wahudumu.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hicho Mhandisi Aadil Hamami, amesema: “Maandalizi ya kuhudumia mazuwaru yalianza muda mrefu, kabla ya kuingia mwezi wa Muharam, tulianza kugawa chakula milo mitatu (asubuhi, mchana na jioni) kuanzia siku ya kwanza, sambamba na kugawa matunda na maji baridi ya kunywa wakati wote bila kusimama”.

Akafafanua kuwa: “Huduma zilikua zinaongezeka kila siku hadi siku ya nane na zilizofuata baada yake, kazi ilikua kubwa kutokana na maukibu nyingi kushughulika zaidi na shughuli za uombolezaji, tuliendelea kugawa chakula hadi siku ya mwezi kumi na tatu, siku ya kukumbuka kuzikwa kwa muili wa Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake, siku ambayo huwa na ushiriki mkubwa wa makabila ya ndani na je ya mkoa wa Karbala”.

Akabainisha kuwa: “Mgahawa haukuishia kutoa huduma ya chakula pekeyake, umeshiriki pia katika shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuzipa mawakibu vitu walivyokua wanahitaji katika shughuli zao, kuandaa gari maaluma iliyokua inasambaza maji baridi ya kunywa, husunan siku ya matembezi ya Towareji, tuligawa maelfu ya grasi za maji ya kunywa kutoka katika kiwanda za maji kilicho chini ya Ataba tukufu”.

Kumbuka kuwa vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya kazi mbalimbali katika mwezi mtukufu wa muharam, na huhakikisha vinatoa huduma bora kwa mazuwaru, wakitumia kauli mbiu isemayo: (kuhudumia mazuwaru ndio utukufu wetu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: