Riwaya zinaonyesha kuwa kichwa cha Imamu Hussein (a.s) kilisoma Qur’ani tukufu katika maeneo tofauti, ikiwa ni pamoja na zilizotajwa na mhakiki Sayyid Abdurazaaq Mugarram katika kitabu cha Maqtal: “Mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) aliendelea kuwa pamoja na Qur’ani, hakika yeye ni mmoja wa vizito viwili alivyo sema Mtume (s.a.w.w) kuwa havitatengana, hivyo Imamu Hussein (a.s) alikua anasoma Qur’ani katika Maisha yake yote hadi baada ya kufa kwake”.
Amepokea Abu Mikhnafi kutoka kwa Shaabi kuwa kichwa cha Imamu Hussein (a.s) kilisulubiwa katika mji wa Kufa, kikasoma surat Kahfi hadi aya isemayo: (… Hakika wao ni vijana waliomuamini Mola wao tukawazidishia uongofu), jambo hilo halikuwaongezea ispokua upotevu.
Katika mapokezi mengine, kichwa kilisulubiwa juu ya jiwe kikasikika kikisoma: (.. Watajua waliodhulumu yapi mafikio watakayo fikia), kilipo fikishwa Damaskas kilisikika kikisema: Laa quwwata illa billahi.
Kilisikika pia kikisoma: (Bali unadhani ya kwamba wale watu wa pangoni na waandishi walikua ni ajabu miongoni mwa ishara zetu?) Zaidu bum Argam akasema: Jambo lako ni ajabu zaidi ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Faadhil Darbandi anasema katika kitabu cha (Asraaru-Shahada) kutoka kwa Muslimah bun Kuhaili: Niliona kichwa cha Hussein (a.s) juu ya mkuki kikiwa kinasoma: (Na Mwenyezi Mungu atakutosheni na yeye ndiye msikivu, mjuzi) Baqarah – 137.
Mshairi anasema:
Ajabu ya kichwa chako juu ya mkuki kimefunikwa na vazi la nuru yako.
Kinasoma kitabu chuu ya mikuki hakika walichoweka juu ya mikuki ni kitabu.