Chuo kikuu cha Alkafeel kinatoa chanjo ya Korona

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa chanjo ya Korona kwa wanafunzi, walimu na watumishi wake, kwa kushirikiana na idara ya afya ya Najafu, kwa ajili ya kulinda afya za watumishi wake na kujiandaa kurudisha mahudhurio ya wanafunzi madarasani mwakani.

Rais wa chuo Dokta Nurisi Dahani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa, “Utoaji wa chanjo ni sehemu ya maelekezo ya wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, kwani mwaka huu wanafunzi watahudhuria madarasani kama kawaida jambo linalo pelekea kuchukua tahadhari zaidi, ikiwa ni pamoja na kupata chanjo”.

Akaongeza kuwa: “Kulikua na mawasiliano ya karibu na idara ya afya ya Najafu, iliyotoa chanjo nyingi zinazo tosha kutolewa kwa watumishi wote, wameanza kupewa chanjo kwa zamu, hali kadhalika idara ya afya imetoa madaktari wa kusimamia zowezi hilo, muitikio ni mzuri tangu siku ya kwanza”.

Akamaliza kwa kusema: “Lengo la kutoa chanjo hii ni kulinda afya na usalama wa watumishi wa chuo na familia zao, na kuzuwia usambaaji wa virusi hivyo katika mwaka huu wa masomo inshallah”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: