Maktaba ya Atabatu Abbasiyya pekee hapa Iraq ni moja ya maktaba nne za kimataifa zilizo pongezwa na (IFLA)

Maoni katika picha
Umoja wa jumuiya na taasisi za maktaba duniani (IFLA), umetuma ujumbe wa kushukuru na kupongeza kituo cha faharasi na kupangilia taaluma kilicho chini ya maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kama moja ya maktba za kimataifa na maktaba pekee hapa Iraq iliyopata pongezi hizo, hii imetokana na kazi kubwa waliyofanya ya kuandika ripoti kuhusu taifa lao, iliyo wekwa kwenye toghuti yake maalum kama mshirika wa kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya 2021m, pamoja na uzowefu wa kushiriki katika mambo ya kimataifa.

Kiongozi wa kituo katika maktaba chini ya kitengo cha habari na utamaduni Ustadh Hasanaini Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Pongezi hizi zimetokana na ushiriki wa kituo cha faharasi na kupangilia taaluma katika ripoti ya taifa iliyo kabidhiwa kwa (VNRS) mara ya kwanza mwaka 2021m, ambapo kazi kubwa imefanywa ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye makongamano na harakati zingine, sambamba na kuchangia katika wizara ya mipango kila tulipo shiriki”.

Mussawi akafafanua kuwa: “Tunaendelea kushirikiana na wizara pamoja na taasisi zenye mafungamano ya swala hili, ripoti hiyo ilikua fursa nzuri ya kutambulisha maendeleo ya maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu, iliyowasilishwa na wizara ya mipango ya Iraq katika kongamano la kimataifa mjini Niyork mwezi wa sita mwaka huu, iliyolenga kuonyesha utekelezaji wa mpango wa maendeleo endelevu wa mwaka 2030m”.

Kumbuka kuwa umoja wa jumuiya na taasisi za maktaba (IFLA) ni taasisi muhimu ya kimataifa inayo angalia maslahi ya maktaba na wanufaika, ni jukwaa linalo unganisha maktaba duniani, inawanachama kutoka nchi (150).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: