Maahadi ya Qur’ani tukufu idara ya wanawake imetangaza kuhitimu wanafuzi katika semina tatu za Qur’ani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaul-Ilmi Lilqur’anil-Karim katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza kuhitimu wanafunzi wa semina tatu ambazo ni (Alhaaniyyah, Riyaadhul-Qur’ani, Faatwimiyyaat), nazo ni semina maalum za kufundisha hukumu za usomaji wa Qur’ani.

Rais wa kitengo cha mitihani katika Maahadi bibi Maasuma Ghulamu Haidari amesema: “Kamati imetoa mitihani ya mwisho kwa wanafunzi (38) walioshiriki kwenye semina tatu za hukumu za usomaji wa Qur’ani, ambazo ni (Alhaaniyya, Riyaadhul-Qur’ani, Faatwimiyyaat)”.

Akaongeza kuwa: “Mitihani inayotolewa na Maahadi ipo ya aina mbili: “Maswali ya nadhariyya kuhusu hukumu za usomaji wa Qur’ani, na maswali ya kujibu kwa vitendo (usomaji) ili kuangalia uwezo wa mwanafunzi katika usomaji”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake linalenga kueneza elimu ya Dini katika jamii ya wanawake, kipaombele cha elimu hiyo ni “maarifa ya Qur’ani”, na kuchangia kuandaa kizazi cha wanawake wanaojua Qur’ani, wenye uwezo wa kusoma na kufanya tafiti katika nyanja zote za Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: