Kuhuisha turathi na kutoa vumbi ni malengo makuu ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendelea na harakati zake bila kusimama, kupitia vituo na idara zake mbalimbali.

Kitengo hiki kinavituo maalum vinavyo husika na kuhuisha turathi za kiislamu, kuzihakiki, kuziandika, kuziweka kwenye faharasi na kuzitangaza, miongoni mwa vituo hivyo ni (kituo cha turathi za Karbala, kituo cha turathi za Hilla, kituo cha turathi za Basra, kituo cha turathi za Najafu, kituo cha turathi za kusini, kituo cha turathi za kiislamu katika mji mtukufu wa Mash-had), aidha kuna idara ya usimamizi wa maarifa na idara ya habari.

Vituo vyote vinawatumishi wenye elimu na uzowefu mkubwa, wameweza kuandika makumi ya vitabu ndani ya miaka michache, na kufanya mikutano mingi ya kimataifa, nadwa za kielimu na warsha, sambamba na kuanzisha vituo vingi vya kimtandao, na kurasa za turathi.

Vituo vya turathi vilivyo chini ya kitengo tajwa vinalenga kuhudumia turathi za kiislamu na kuzienzi pamoja na kuzitoa vumbi, kwa kufanya tafiti, uhakiki na kuandika, kwa lengo la kuzipa maktaba za kiarabu na kiislamu vitabu zaidi, na kuangazia mchango wa miji ya Iraq katika sekta zote za elimu.

Tambua kuwa kitengo cha maarifa huendesha semina na kutoa mihadhara, kwa lengo la kukuza uwezo wa watumishi wake, nacho ni moja ya vitengo vyenye jukumu la kuhuisha turathi za kiislamu na kufichua hazina zilizojificha katika nakala-kale.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: