Kitengo cha Tarbiyya na elimu ya juu kinaendesha shindano la (Siraajul-Ameed) linalo husu watumishi wa shule

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendesha mashindano ya (Siraajul-Ameed) kwa watumishi wa shule.

Kiongozi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Hassan Daakhil amesema: “Shindano la (Siraajul-Ameed) ni sehemu ya kujiandaa na mwaka wa masomo (2021 – 2022m), limeanza tangu wiki iliyopita, linalenga kukuza ushirikiano”.

Akaongeza kuwa: “Shindano hili ni aina nyingine miongoni mwa aina za ufundishaji, linategemea mtindo wa maswali, yanayo lenga kutoa nafasi ya kujadili kielimu kati ya wakufunzi na wanafunzi wa shule za Al-Ameed”.

Akaendelea kusema: “Tunategemea shindano litaendelea kwa muda wa siku tano, kila siku yatashindana madarasa matatu wakiwa pamoja na walimu wao, na kufanyia kazi uzowefu unaopatikana katika zowezi hilo”.

Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu huendesha semina, warsha na mashindano ya kielimu, kwa lengo la kuongeza uwezo wa watumishi wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: