Watumishi wa mazaru ya Suleimani Mhammadiy wanaomboleza kumbukumbu ya kifo cha Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa mazaru ya swahaba mtukukufu Suleimani Muhammadiy (r.a) kwa kushirikiana na Maukibu ya Answaru Sayyidah Rugayyah (a.s) katika mji wa Madaaini, wanakumbuka vita ya Twafu na kuomboleza kifo cha mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake (a.s), mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wakiwa katika maukibu kubwa ya uombolezaji, wamezowea kuja Karbala kuomboleza katika siku kama hizi.

Waombolezaji wamekuja wakiwa vikundi vikundi, wameanzia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imefanywa majlisi ya kuomboleza iliyo husisha usomaji wa kaswida na tenzi za Husseiniyya, zilizo amsha hisia za yaliyojiri kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), katika siku kama hizi juu ya Ardhi hii, miongoni mwa mauaji, unyang’anyi, uchomaji moto mahema na makosa mendine ya kibinaadamu.

Baada ya hapo wakaelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s) kufanya kama walivyo fanya ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), huku wakiimba kaswida za kuomboleza kuuawa kwa Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Uongozi mkuu wa mazaru hiyo umezishukuru Ataba zote mbili kwa mapokezi mazuri waliyopewa.

Kumbuka kuwa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zinaendelea kupokea mawakibu Husseiniyya kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, kuna mawakibu zinaendelea kuja kutoa pole chini ya ratiba ya kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kuanzia kumi la kwanza, la pili na la tatu katika mwezi wa Muharam, zitaendelea kumiminika hadi mwishoni mwa mwezi wa Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: