Kumbukumbu ya kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s)

Maoni katika picha
Siku kama ya leo mwezi ishirini na tano Muharam, ni siku ya tukio linalo umiza, lililotokea katika nyumba ya Mtume mashukio ya wahyi, ni siku aliyokufa kishahidi Imamu Ali bun Hussein Sajjaad (a.s) mwaka wa (94h).

Imamu Zainul-Aabidina (a.s) sehemu kubwa ya Maisha yake alikua anafunga mchana na kuswali usiku, sambamba na kukumbuka yaliyojiri Karbala kwa baba yake na watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), alikua kila anapomuangalia shangazi yake na dada zake anakumbuka kukimbia kwao siku ya twafu, wakitoka kwenye hema hadi hema linguine, na sauti ya watu waliokua wanasema: chomeni hema za madhalimu, jambo hilo lilikua linamhuzunisha sana, hakika jambo hilo lilikua na athari kubwa katika Maisha yake.

Imamu alikua anakubalika sana kwa watu, watu waliongelea elimu yake na ibada zake bila kusahau subira yake na mambo mengine mengi, nyoyo za watu zilimpenda na kumuheshimu, watu walifurahi kumuona na kumsikiliza, jambo hilo liliwaumiza bani Umayya na kuwanyima usingizi, miongoni mwa waliomchukia zaidi ni Walidi bun Abdulmaliki.

Imepokewa kutoka kwa Zuhairi kuwa alisema: Sina raha kwa kuwepo Ali bun Hussein hapa duniani, akapanga njama ya kumuua Imamu baada ya kuchukua utawala, alipochua utawala akatuma sumu kali kwa mtumishi wake na kumuambia wamuwekee Imamu, mtumishi huyo akatekeleza agizo hilo, Imamu akapewa sumu iliyo muuguza kwa siku kadhaa, watu wakawa wanaenda kumuangalia wakati wa maradhi yake (a.s), wanamkuta anamsifu Mwenyezi Mungu na kumshukuru kwa kumruzuku kifo kinachotokana na kiumbe muovu.

Imamu Abu Jafari Baaqir akaandaa muili mtakatifu wa baba yake, watu wakakuta sugu kubwa kwenye viungo vya kusujudia kutokana na wingi wa kusujudu kwake, wakaangalia mabega yake yalikua na sugu kama vile za magoti ya ngamia, wakamuuliza Imamu Baaqir (a.s) kuhusu sugu hizo, akawaambia: Zinatokana na mifuko ya chakula aliyokua anabeba kwenye mabega hayo na kwenda kugawa kwa mafukara usiku, baada ya kumaliza kumuosha walimvisha sanda na kumswalia.

Imamu alizikwa na umati mkubwa sana wa watu, ambao ulikua haujawahi kutokea katika mji wa Madina, jeneza lake lilishindikizwa na watu wema na waovu, kila mtu alisikitika kwa kifo chake na kumlilia, ilionekana wazi hasara kubwa kwa kifo chake, walipoteza heri nyingi ikiwa ni pamoja na mazingira bora ya kiroho yasiyokua na mfano, kila mtu alijitokeza kwenda kushindikiza muili wake mtakatifu.

Muili huo mtukufu ukapelekwa hadi katika makaburi ya Baqii, wakamzika karibu na kaburi la Ammi yake Imamu Hassan bwana wa vijana wa peponi, mjukuu wa Mtume (s.a.w.w), Imamu Baaqir (a.s) akalaza muili wa baba yake katika nyumba yake ya mwisho, hakika alilala na elimu, wema, taqwa na rohaniyya ya Mitume na wachamungu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: