Muhimu: Kuanza ushindikizaji wa muili wa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Muhammad Saidi Hakim

Maoni katika picha
Ushindikizaji wa muili wa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Muhammad Hakim umeanza katika Atabatu Husseiniyya tukufu, kundi kubwa la viongozi wa Dini na wawakilishi wa ofisi za Maraajii Dini kutoka Najafu na wanafunzi wa hauza pamoja na wananchi kwa ujumla wameshiriki.

Waombolezaji wamekusanyika katika malalo ya babu yake Imamu Hussein (a.s), ambapo wamepokewa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai na watumishi wa malalo hiyo takatifu, wamefanya ibada ya ziara na kusoma dua mbele ya kaburi takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: