Ataba mbili tukufu zimepokea muili wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Muhammad Saidi Hakim ukishindikizwa na umati mkubwa wa watu

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Asubuhi ya Jumamosi (26 Muharam 1443h) sawa na (4 Septemba 2021m), zimepokea muili wa Faqihi Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Muhammad Saidi Hakim, aliyefariki siku ya jana kwa maradhi ya moyo.

Ameshindikizwa na umati mkubwa wa viongozi wa Dini na wawakilishi wa ofisi za Maraajii Dini katika mji wa Najafu na wanafunzi wa hauza na wanajamii kwa ujumla.

Msafara wa kumshindikiza ulianzia katika malalo ya babu yake Imamu Hussein (a.s), wamepokewa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya tukufu, Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai na watumishi wa malalo hiyo takatifu, halafu wakaswalia jeneza, swala hiyo ikaongozwa na Sayyid Muhammad Taqi Hakim ndugu wa Marjaa aliyefariki, kisha wakafanya ibada ya ziara na wakasoma dua iliyo ongozwa na Shekh Karbalai, halafu muili wake ukazungushwa katika kaburi takatifu.

Kisha ukabebwa kwa huzuni na majonzi makubwa na kuelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambako walipokewa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na makamo wake na marais wa vitengo vya Ataba, bila kuwasahau watumishi wa Abulfadhi Abbasi (a.s), halafu wakafanya ibada ya ziara kwa niaba ya marehemu, iliyo ongozwa na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kisha wakafanya majlisi ya kuomboleza na mwisho akazungushwa katika malalo hiyo takatifu.

Halafu washindikizaji wakabeba muili na kuelekea katika mkoa wa Najafu kwa ajili ya mazishi. Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu ilijiandaa kupokea msafara wa washindikizaji wa muili huo mtukufu toka jana mchana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: