Zaidi ya maukibu 100 zinaingia katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya jana siku ya Jumamosi (26 Muharam 1443h) sawa na tarehe (4 Septemba 2021m), mawakibu za kuomboleza kutoka katika mji wa Hilla zimewasiri katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), idadi ya maukibu hizo ilifika (111), kutoka vitongoji tofauti vya mkoa wa Baabil, haya ndio mazowea yao katika uombolezaji, hufanya sambamba na kumbukumbu ya kifo cha Imamu Sajjaad (a.s).

Uingiaji wa mawakibu za (Zanjiil na matam) ulifuata ratiba maalum, iliyopangwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kwa ajili ya kurahisisha matembezi yao na kutokwamisha shughuli za mawakibu zingine au mazuwaru.

Rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kuwasili mawakibu katika wakati huu na kwa idadi kubwa kiasi hiki, ni muendelezo wa kuomboleza tukio la Twafu la kuuawa Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake sambamba na kuomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s), kwani asilimia kubwa ya maukibu hizo zinajiandaa kutoa huduma kwa mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala, hicho ndicho hufanywa na mawakibu hizo na ndio tofauti ya maukibu hizi na zingine”.

Akafafanua: “Maukibu hizo zilizo jiunda kwa makundi ya waombolezaji, kila moja ilianza matembezi yake sehemu iliyopangiwa kutokana na kitongoji au mtaa wanakotoka katika mkoa wa Baabil, walianzia katika barabara ya Baabul-Qibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi ndani ya haram yake tukufu, kisha walielekea katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, na kumaliza matembezi yao ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s), matembezi yote yanasimamiwa na watumishi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, kwa ajili ya kupangilia matembezi hayo”.

Wakati wa matembezi zimeibwa kaswida na tenzi za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni ya msiba wa Ashura, na yaliyowatokea Ahlulbait (a.s) na mashukio ya wahyi, pamoja na kutekwa familia ya Imamu Hussein (a.s) na yaliyo endelea kujiri kwao katika siku kama hizi mwaka wa 61h, sambamba na kuomboleza kifo cha Imamu Ali Sajjaad (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: