Kuna kisa gani cha tone la damu ya kichwa kitukufu cha Imamu Hussein (a.s) ambapo imejengwa Maqaam?

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa msafara wa mateka wa Imamu Hussein (a.s) na vichwa vitakatifu, katika siku kama hizi kuna sehemu walisimama, nayo ni katika mji wa Mosul uliopo pembezoni mwa mto wa Dujla kaskazini mwa Iraq, upo umbali wa (kilometa 600) kutoka Kufa.

Katika kitabu cha (Nafsul-Mahmuum) imeandikwa kuwa: “Watu waliokua katika msafara wa mateka wa Imamu Hussein (a.s) walipotaka kuingia katika mji wa Mosul walituma ujumbe kwa kiongozi wa mji huo awaandalie mapokezi na kusafisha mji, watu wa Mosul wakakubali na kuwaomba wasiingie katika mji huo hadi watakapo maliza maandalizi ya kuwapokea, msafara ukasimama umbali wa Farsakh moja, wakaweka kichwa kitukufu cha Imamu Hussein juu ya jiwe, damu ya kichwa hicho kitakatifu ikadondokea juu ya jiwe hilo, ikawa kila mwaka inapofika siku ya Ashura damu inachemka kwenye jiwe hilo, watu wakawa wanakusanyika hapo na kuomboleza kila mwaka, hali hiyo iliendelea hadi wakati wa utawala wa Abdulmaliki bun Marwani, akaamuru jiwe litolewe, baada ya kutolewa damu haikuonekana tena, ndipo ikajengwa Maqaam iliyopewa jina la Mash-hadu Nuqtwah”.

Katika kitabu cha (Alkaamil) imeandikwa kuwa: “Wabeba kichwa kitakatifu walikua wanaogopa magabila ya waarabu wasije kuwanyang’anya kichwa hicho, wakaacha kupita njia maarufu na kupita njia zisizo julikana, kila walipofika katika Kijiji walisema hiki ni kichwa cha Khawariji”.

Katika sehemu nyingine imetajwa kuwa -kuhusu sababu za kujengwa Mash-hadu hiyo- baada ya kuuawa Imamu Hussein (a.s) kichwa chake kilipelekwa Sham, wakapita sehemu ya Dairu-Saidi, wakasimama katika Kijiji cha karibu na sehemu hiyo, kichwa cha Imamu Hussein (a.s) kilikua katika mfuko, mmoja wa Makasisi wa mji wa Dairu akatambua kuwa wamebeba kichwa cha Imamu Hussein (a.s), akakichukua na kukiosha kisha akakipaka marashi, akakaa nacho siku moja, teno la damu likadondoka katika ardhi kilipo lala, Kasisi hiyo akajenga Mash-Hadu sehemu hiyo, ikaitwa Mash-Hadu Nuqtwatul-Hussein, ikawa sawa na makumbusho kwa watu wa Mosul.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: