Baada ya kumaliza kutengenezwa kwake: Imeanza kazi ya kuunganisha vipande vya dirisha la Maqaam ya mkono katika kiwanda cha kutengeneza madirisha ya kwenye makaburi

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha kutengeneza madirisha ya kwenye makaburi na milango mitukufu katika Atabatu Abbasiyya, wameanza kufunga dirisha la Maqaam ya mkono wa kushoto wa Abulfadhil Abbasi (a.s), ndani ya kiwanda cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naadhim Ghuraabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya kumaliza kutengeneza vipande vyote vya dirisha ikiwa ni pamoja na sehemu za madini na mbao, na kukamilisha maandalizi ya kuliweka sehemu yake ambayo ipo jirani na haram tukufu, tumeanza kufunga vipande vya dirisha, kazi ambayo ni sehemu ya hatua za utengenezaji wa dirisha hilo, baada ya kumaliza litafanyiwa ukaguzi wa mwisho na kujiridhisha, kisha litafunguliwa na kwa ajili ya kuwekwa madini ya mina na dhahabu, na kazi zingine ambazo haziwezi kufanywa likiwa katika hali hii”.

Akaongeza kuwa: “Hatua ya ufungaji wa pili itafanywa baada ya kumaliza kuweka mina, dhahabu, mapambo na nakshi, kama mchoro unavyo onyesha sambamba na kuchukua tahadhari ya jambo lolote linaloweza kujitokeza, hii ndio kazi tunayofanya kwa sasa”. Akafafanua kuwa: “Baada ya kazi hii viongozi wa Ataba watakuja kukagua na kutoa maoni yao, ndio litakapo funguliwa na kuweka namba kila kipande kitakachowekwa madini au mbao, kisha kukamilisha matengenezo ya kila sehemu, kazi ambayo hufanywa kwa umahiri na umakini mkubwa”.

Kumbuka kuwa dirisha linapembe nane, nalo ni dirisha la kwanza kutengenezwa kwa umbo hili, linamzunguko wa (mita 3) na urefu wa (mita 2.85) linasilva yenye ujazo wa (mlm 2), limetengenezwa kwa umakini mkubwa na ufundi wa hali ya juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: