Kuanza kwa safari ya wanaokwenda kwa Hussein (a.s) kutoka baharini hadi mtoni

Maoni katika picha
Mji wa Ra-asu Shaiba katika mkoa wa Basra uliopo umbali wa (klm 675) kutoka Karbala, umeshuhudia kuondoka kwa msafara wa kwanza unaoenda kuzuru malalo ya Imamu Hussein (a.s) katika kuhuisha kumbukumbu ya Arubaini, msafara huo umeondoka asubuhi ya leo siku ya Jumanne (29 Muharam 1443h) sawa na tarehe (6 Septemba 2021m).

Msafara huo unafanywa kwa mwaka wa tisa mfululizo, hivyo imeandaliwa hafla ya uzinduzi wa matembezi ya Arubaini chini ya kauli mbiu isemayo: (Kutoka baharini hadi mtoni) inayo ongozwa na taasisi ya maadhimisho chini ya ofisi ya Marjaa Dini aliyefariki Sayyid Muhammad Saidi Hakiim (q.s) kwa kushirikiana na vikundi vya mawakibu Husseiniyya katika mji wa Basra pamoja na taasisi za serikali na watu wa wilaya ya Faao, imehudhuriwa na viongozi wa Dini na kijamii pamoja na mazuwaru.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Shekh Faisal Abadi amesema: “Ilikua inatakiwa mzungumzaji wa kongamano hili atokane na familia ya Aali Hakiim, lakini tumeshtushwa na kifo cha Marjaa Dini mkuu Sayyid Muhammad Saidi Hakiim, hivyo wameshughulishwa na kumuandaa, kumshindikiza na kumzika, katika kuyafanyia kazi aliyotufundisha Marjaa huyo mtukufu, swala la Imamu Hussein (a.s) na maombolezo haya, ndio sababu kubwa ya kuendelea kuwepo kwa madhehebu hii tukufu, pia ni jambo linalotukurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Akafafanua kuwa: (Mwenyezi Mungu mtukufu ametuneemesha kwa kumtambua na kumtambua Mtume wake na Ahlulbait (a.s), katika kudumisha neema huyo na kumshukuru yatupasa mushikamana na mafundisho ya Mtume na watu wa nyumbani kwake, yanayo himiza kuhuisha mambo yao, likiwemo tukio la Imamu Hussein (a.s), na kukuza mshikamano pamoja naye (a.s) kupitia matembezi ya kwenda kuzuru kaburi lake na kuhudumia watu wanaokwenda kumtembelea”.

Akamaliza kwa kusema: “Hakika kuhuisha na kukumbuka tukio hili kunathawabu nyingi mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, kwani ni kumliwaza Mtume na watu wa nyumbani kwake akiwemo Imamu Zainul-Aabidina na shangazi yake bibi Zainabu (a.s), kutokana na matatizo waliyopata katika siku kama hizi mwaka wa (61h)”.

Kongamano limeshuhudia uimbwaji wa kaswida na mashairi ya Husseiniyya, aidha imepandishwa bendera maalum nyeusi iliyo andikwa (matembezi ya uaminifu kwa Hussein kutoka baharini hadi mtoni), matembezi yanaanzia kusini mwa Iraq katika mji wa Faao hadi sehemu alipouawa Imamu katika mji wa Karbala, kama tangazo la kuondoka msafara wa kwanza wa matembezi ya mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: