(Qur’ani tukufu agizo la Imamu wa zama) anuani ya nadwa iliyofanywa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Baabil

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaul-Ilmi Lilqur’anil-Kariim katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya nadwa ya kielimu chini ya anuani isemayo: (Qur’ani tukufu agizo la Imamu wa zama).

Kiongozi wa tawi Sayyid Muntadhir Mashaaikhi amesema: “Mhadhiri wa nadwa alikua ni Dokta Ali Abdulfataah Alhasanawi, akabainisha jinsi anavyo angalia Imamu Mahadi (a.f) Qur’ani tukufu na kuilinda.

Akasisitiza kuwa: “Huu ni muendelezo wa nadwa zingine za kielimu zinazofanywa na Maahadi kwa wanafunzi wake, kwa lengo la kupanua wigo wa fikra” akabainisha kuwa: “Imepata muitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi wa Maahadi”, akasema: “Nadwa hii ni sehemu ya mradi wa kielimu unaofanywa na Maahadi katika mkoa wa Baabil”.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil hufanya nadwa za Qur’ani na harakati zingine zinazo lenga kufundisha utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya vizito viwili katika jamii.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu na matawi yake ya mikoani, huendesha miradi mingi ya kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: