Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil inafanya mradi wa kutoa mihadhara majumbani

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majma-ilmi lilqur’anil-kariim katika Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha mradi wa mihadhara majumbani kwa waumini.

Mradi huu unaongozwa na wasomi wa Fiqhi, Aqida na sekula, baada ya kuchagua mada mapema katika idara ya tawi la Maahadi, aidha mradi unakusudia kufundisha vizito viwili Qur’ani na kizazi kitakatifu, wanatumia aya za Qur’ani tukufu na riwaya za Ahlulbait (a.s) katika kuandaa masomo ya kimaadili.

Mradi umepata muitikio mkubwa kutoka kwa wakazi wa mkoa wa Baabil, wamesema kuwa ni hatua kubwa inayosaidia kueneza mafundisho ya Qur’ani katika mji huu.

Tambua kuwa mradi utadumu kwa muda wa miezi miwili, Muharam na Safar hapa mkoani.

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil, hufanya harakati mbalimbali pamoja na kuendesha semina za Qur’ani mfululizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: