Bendera ya ukarimu wa Husseini inapepea kama alama ya kuanza msimu wa Arubaini

Maoni katika picha
Jioni ya Jumatano kwa mwaka wa kumi na nne mfululizo inafanywa shughuli ya kupandisha bendera ya ukarimu wa Husseini katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa nje, uliopo katika barabara ya (Najafu – Karbala) kama alama ya kuanza kuhudumia mazuwaru.

Mjumbe wa kamati kuu katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Jawadi Hasanawi amesema: “Ni kawaida ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupandisha bendera hiyo katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa nje kila mwaka, kama ishara ya kuanza kutoa huduma kwa mazuwaru wanaotembea kutoka (Najafu – Karbala), mgahawa huo ni mingoni mwa vituo muhimu kwa mazuwaru”.

Naye kiongozi wa mgahawa Sayyid Kaadhim Twahir Mussawi amesema: “Mgahawa unahudumia mazuwaru wakati wote wa mwaka, lakini katika ziara ya Arubaini kazi huongezeka kutokana na kuingia mamilioni ya watu katika mji wa Karbala na wengi wao wakitumia barabara hii ya (Najafu – Karbala)”.

Akaongeza kuwa: “Kuanzia (tarehe 1) hadi (20 Safar) mgahawa hutoa huduma zote, chakula, vinywaji, malazi pamoja na huduma za afya” akasema: “Mgahawa unasehemu ya wanaume na wanawake”.

Kumbuka kuwa bendera hupandishwa juu ya mlingoti wenye urefu wa mita (40), bendera inaupana wa mita (13) na urefu wa mita (17), imeandikwa pande zote mbili kwa wino mwekundu neno lisemalo: (Amani iwe juu yako ewe mbeba bendera ya Hussein -a.s-).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: