Mwezi mosi Safar kuwasili kwa mateka wa Imamu Hussein (a.s) na kichwa chake kitukufu katika mji wa Sham

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa mwezi mosi Safar mwaka 61 hijiriyya, msafara wa mateka wa Imamu Hussein (a.s) pamoja na kichwa chake uliwasiri katika mji wa Damaskas, walipo karibia kuingia katika mji wa Damaskas Ummu-Kulthum alimuomba Shimri awaweke katika kundi lisilo angaliwa sana, wasitembee pamoja na wabeba vichwa, ili watu washughulishwe zaidi na kuangalia vichwa na sio wao, hakika walitembea katika hali ambayo muili unasisimka kuitaja, aliamuru watembee sehemu wanayo angaliwa zaidi na wabeba vichwa wakae katikati yao.

Walipo fika langoni akawasimamisha kwa muda, watu wakiwa wanapiga dufu kwa shangwe na furaha, mtu mmoja akamsogelea Sukaina akasmea: Nyie mateka wa wapi? Akamjibu: Sisi ni mateka kutoka katika familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Mzee mmoja akamfuata Imamu Sajjaad (a.s) akasema: Namshukuru Mwenyezi Mungu aliyekuangamizeni na kumuwezesha kiongozi dhidi yenu, Imamu akaonyesha hekima yake katika kumueleza yule mzee na kumuonyesha njia sahihi, hivyo ndio walivyo watu wa nyumba ya Mtume (a.s), nuru zao huchomoza kwa kila mtu mwenye moyo safi na utayali wa kuongoka, akasema (a.s): “Ewe Mzee unajua kusoma Qur’ani?” akasema: Ndio, akasema (a.s): “Umesoma aya isemayo (Sema sikuombeni malipo juu yake ispokua kuwapenda jamaa zangu wa karibu)? Na aya isemayo: (Na wapeni jamaa wa karibu haki yao)? Na aya isemayo: (Tambueni chochote mnachopata katika ngawira, hakika khumsi (asilimia tano yake) ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume na jamaa wa karibu)? Yule Mzee akasema ndio nazijua aya zote hizo. Akasema (a.s) “Wallahi sisi ndio jamaa wa karibu tunaotajwa kwenye aya hizo”.

Kisha Imamu akamuambia: “Umesoma kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: (Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na kukutakaseni mtakaso)? Akasema: Ndio. Akasema (a.s): Sisi ndio watu wa nyumba ya Mtume tuliokusudiwa kwenye aya hiyo” yule mzee akasema: Namuapa Mwenyezi Mungu juu yako, ndio nyie? Akasema (a.s): Namuapa Mwenyezi Mungu kwa haki ya babu yangu Mtume wa Mwenyezi Mungu sisi ndio hao, bila shaka yeyote”.

Yule mzee akaanza kubusu miguu yake huku anasema: Najilinda kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya waliokuuweni, akaendelea kuongea maneno ya kuomba toba mbele ya Imamu, taarifa ikafika kwa Yazidi kuhusu mzee huyo, akaamuru auawe.

Yazidi alikua amekaa katika Qasri yake, alipoona mateka wanaingia na vichwa vikiwa juu ya mikuki, wanaingia kwenye mpaka wa mji wa Jairun (Damaskas), akasema:

Walipo chomoza wale watu na vile vichwa katika mpaka wa Jairun.

Nikasema, sema au usiseme nimelipa deni langu kwa Mtume.

Kabla ya kuingia msafara kwa Yazidi, walichukua kamba na kumfunga shingoni, Zainul-Aabidina (a.s) iliyo mfunga Zainabu na Ummu-Kulthum pamoja na mabinti wengine wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), kila walipo punguza mwendo walipigwa hadi wakafikishwa mbele ya Yazidi, aliyekua amekaa juu ya kitanda chake, Ali bun Hussein (a.s) akasema: “Unadhani Mtume atafanyaje akituona tupo katika hali hii?) watu waliokuwepo wakalia, Yazidi akaamuru wafunguliwe kamba, na wasimamishwe mbele ya mlango, sehemu ambayo husimamishwa mateka, kichwa kitakatifu kikawekwa mbele ya Yazidi, akawa anawaangalia na kusema:

Tulisubiri na Subira kwetu ilikua ngumu panga zetu hukata watu muhimu

Hutenganisha vichwa vya watu watukufu ambao kwetu ni waovu na madhalimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: