Zaidi ya wanafunzi 350 wanashiriki katika matembezi ya kuomboleza na hafla ya Qur’ani

Maoni katika picha
Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule, kwa kushirikiana na Majmaa-Ilmul Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeratibu program ya Qur’ani na kumboleza ambayo wameshiriki Zaidi ya wanafunzi (350) kutoka vyuoni na kwenye shule za sekondari, ndani na nje ya mkoa wa Karbala, anuani ya program hiyo ilikua inasema, uhusiano wa Imamu Hussein (a.s) na harakati yake ya milele katika kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu, jioni ya jana siku ya Jumatano (30 Muharam 1443h) sawa na tarehe (8 Septemba 2021m).

Matembezi yalianzia katika haram ya Aqilah Zainabu (a.s) katika mfumo wa vikundi, wakisimama kila chuo au shule katika kikundi chao, kisha wakaelekea katika malalo ya Imamu Hussein (a.s) na kusimama mbele ya kaburi lake takatifu, na kutoa pole kwa kutumia maneno ya huzuni yanayo onyesha ukubwa wa msiba huo.

Baada ya hapo wakaelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, walipo fika huko wakafanya majlisi ya kuomboleza ambayo watumishi wa Ataba hiyo pia walishiriki, tenzi za kuomboleza zimesomwa na Muhammad Amiri Tamimi, kutokana na msiba huu mkubwa uliohuzunisha moyo wa Mtume na binti yake bibi Zaharaa (a.s), na kuwaliza watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wapenzi wao.

Halafu ikafanywa hafla ya usomaji wa Qur’ani, iliyo funguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na Muslim Shabaki, kisha ikasomwa kaswida ya kimashairi na Hamza Samawi.

Wakafuata wasomaji wengine walioburudisha masikio ya wahudhuriaji, miongoni mwa walio soma ni: Msomaji wa Ataba mbili tukufu bwana Osama Karbalai, na Dokta Ahmadi Najafiy kutoka Atabatu Alawiyya tukufu, na kutoka katika Maahadi ya Qur’ani tukufu akasoma Sayyid Haidari Jaluhani Mussawi, wakamalizia kwa kusoma Ustadh Aamir Alkaadhimiy.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: