Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake yazindua semina mpya

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya imetangaza kuanza kwa semina sita mpya za Qur’ani, zinazo jikita katika ufundishaji wa hukumu za usomaji wa Qur’ani, zenye majina yafuatayo (Dhariyaat, Jalaaul-Quluub, Baswaairul-Qur’ani, Sayyidat Maryam, Salsabiil, Sayyidat Aasiya).

Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi amesema: “Wanagawa wanafunzi katika makundi kulingana na umri wao, semina ya (Jalaaul-Quluub na Sayyidat Aasiya) kwa wanafunzi wa sekondari (upili)”. Akaongeza kuwa “Semina ya “Dhaariyaat na Sayyidat Maryam) kwa wanafunzi wa chuo, na semina ya (Baswaairul-Qur’ani na Salsabiil) kwa wanafunzi waliojuu ya miaka ya chuo, sambamba na kuzingatia kiwango cha elimu katika kila kundi kulingana na selebasi ya Maahadi”.

Akafafanua kuwa: “Semina zitafanywa kwa njia mbili, uhudhuriaji na mtandao, kwa lengo la kufikisha elimu ya Qur’ani kwa watu wengi zaidi, na kutoa huduma kwa waumini wa kike hata kama wako mbali, bila kuwepo darasani”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake chini ya Majmaa-Ilmul Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kusambaza elimu ya Dini kwa wanawake, ikiwemo elimu ya Qur’ani, na kuchangia katika kutengeneza kizazi cha wasomi wenye uwezo wa kufanya tafiti katika sekta tofauti za Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: