Idara ya Tahfiidh inafanya shindano la kila mwezi kwa wanafunzi wake wa Karbala

Maoni katika picha
Idara ya Tahfiidh chini ya Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefanya shindano la mwisho wa mwezi kwa wanafunzi wa tahfiidh kwa lengo la kuongeza uwezo wao.

Shindano hilo limefanyiwa ndani ya jingo la Alqami chini ya Atabatu Abbasiyya, wameshiriki wanafunzi waliofanya vizuri katika kuhifadhi.

Shindano linasaidia kutambua wanafunzi waliohifadhi vizuri miongoni mwa washiriki, aidha linasaidia kutambua kazi kubwa inayofanywa na walimu.

Shindano hili ni sehemu ya kujiandaa na kushuriki mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni kituo muhimu cha elimu ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, inajukumu la kusambaza elimu ya Qur’ani na kuandaa jamii yenye uwelewa mzuri wa Qur’ani katika kila sekta.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: