Karibia na ziara ya Arubaini.. Chuo kikuu cha Al-Ameed kinajiandaa kutoa huduma maalum kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed kinaandaa maukibu ya Ummul-Banina (a.s), itakayo toa huduma ya kupokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubaini ijayo.

Maukibu ya Ummul-Banina (a.s) hutoa huduma tofauti kwa mazuwaru, hususan wanaopita barabara ya (Najafu – Karbala), maukibu hiyo hutoa huduma ya maelekezo, utamaduni, tiba, malazi, chakula, vinywaji na zinginezo.

Kumbuka kuwa maukibu ya Ummul-Banina (a.s) katika chuo kikuu cha Al-Ameed, hutoa huduma kwa mazuwaru wa Karbala katika kila msimu wa ziara ya Arubainiyya, pia ni moja ya vituo ambavyo hupitia mazuwaru wanaotembea kupitia barabara ya (Najafu – Karbala).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: