Kuanza kwa kongamano la Imamu Hassan Almujtaba (a.s) awamu ya nane

Maoni katika picha
Chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na kamati ya miradi ya Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) na jumuiya ya kielimu Al-Ameed na chuo cha Alkafeel na Al-Ameed na idara ya malezi ya mji wa Baabil, asubuhi ya Alkhamisi tarehe (9/9/2021m) sawa na (1 Safar 1443h), vimeanza vikao vya kongamano la Imamu Hassan (a.s) la mwaka wa nane, chini ya anuani isemayo: (Turathi za Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika masomo ya kibinaadamu utafiti wa rai na rai nyingine), kongamano linafanywa kwa kuhudhuriwa na washiriki katika chuo kikuu cha Baabil ndani ya ukumbi wa Shahidi Muhammad Baaqir Swadr.

Kongamano limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na “Yusufu Hakiim Albakri” kutoka uongozi maalum wa mazaru ya Alawiyyah Sharifah bint Imamu Hassan (a.s), kisha ukaibwa wimbo wa taifa na wimbo wa Ataba tukufu (Lahnul-Ibaa) halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi na wanachuoni, kisha akaongea muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Riyaadh Twaariq Al-Amiidi ambaye pia ni muwakilishi wa jumuiya ya kielimu Al-Ameed, miongoni mwa aliyosema ni: “Amani ya Mwenyezi Mungu na rehema zake na baraka zake ziwe juu yenu… salamu imefungamana na dua njema kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu, wanashukuru kupata mualiko wenu mtukufu, nao wameitikia haraka bila kusita na wako tayali kutoa mchango wowote unaohitajika katika kutangaza haki na kuonyesha mapenzi kwa Ahlulbait (a.s) sambamba na kusambaza mafundisho yao na kuhuisha mambo yao, bila shaka mambo hayo yako chini ya ridhaa ya mkarimu wa Ahlulbait Imamu Hassan -a.s”.

Akaongeza kuwa: Bwana wangu ewe Mujtaba bwana wangu ewe Twayyib ewe mtoto wa watu wema, kutokana na ukarimu wenu na utukufu wenu, nafsi zote hizi tukufu zimekuja mbele ya mlango wenu zinapiga hodi zikiwa na kiu kali ya kua karibu yenu.

Akaendelea kusema: Watukufu wahudhuriaji Mwenyezi Mungu awawafikishe… mafundisho ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) ni muhimu kwa binaadamu wote, ndio maana anuani ya kongamano hili inasema (Turathi za Imamu Hassan Almujtaba “a.s” katika masomo ya kibinaadamu: tafiti katika rai na rai nyingine). Miongoni mwa malengo ya kongamano hili ni:

Kusafisha turathi za zamani zilizochafuliwa na wanahabari waovu wa zamani na wasasa, kwa kueleza ukweli halisi na kubaini uongo na ukweli, hilo ndio jukumu la kongamano hili… na mwisho wa dua zetu husema kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu mtukufu na rehema na amani ziwe juu ya Mtume Muhammad na Aali wake watakatifu.

Halafu ukafuata ujumbe wa kamati ya miradi ya Hilla Mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), ulio wasilishwa na Mhandisi Astashari (Hassan Alhilliy), waheshimiwa wahudhuriaji watukufu na wageni kutoka Ataba tukufu pamoja na wageni wengine wote.. Mheshimiwa Rais wa chuo kikuu cha Baabil tunawakaribisha kwa heshima kubwa katika ufunguzi wa kongamano la Imamu Hassan Almujtaba (a.s), mwaka huu litafanywa kwa muta wa siku tatu kwenye mikoa mitatu tofauti, chini ya uongozi wa Ataba mbili tukufu, siku ya kwanza ambayo ni maalum kwa tafiti za kisekula, inafanywa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Baabil kitivo cha malezi na elimu za kibinaadamu, na idara ya malezi na elimu za kibinaadamu katika mkoa wa Baabil na uongozi maalum wa mazaru ya Alawiyya Sharifa mtoto wa Imamu Hassan (a.s) na kituo cha kimataifa Al-Ameed kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Akasema: Siku ya pili itakua katika mkoa wa Najafu kwa kushirikiana na Majmaa Imamu Almurtadha (a.s), nayo ni maalum kwa mada za kihauza, na siku ya tatu itakua katika mkoa wa Karbala ambayo ni maalum kwa mashairi, itafanywa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Akamaliza kwa kusema: Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuwezeshe kufanya harakati zingine ndani ya kongamano hili tukufu, shukrani za pekee ziwaendee viongozi wakuu kisheria katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya hususan Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi anaye tusaidia bila ukomo pamoja na vitengo vyote vya Ataba tukufu kwa kazi kubwa waliyofanya ya kufanikisha kongamano hili.

Baada ya hapo ikawasilishwa mada ya ufunguzi na Dokta Abbasi Ali Hussein Alfahaam kutoka chuo kikuu cha Kufa/ kitivo cha malezi ya wasichana, iliyokua na anuani isemayo (Imamu Hassan (a.s) adabu ya sera na khitwabu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: