Kongamano la Imamu Hassan (a.s) la nane: linahitimisha vikao vyake kwa mzungumzaji wa lugha ya kiengereza

Maoni katika picha
Jioni ya Alkhamisi tarehe (9/9/2021m) sawa na (1 Safar 1443h), kikao cha nne kilihitimishwa na mzungumzaji wa lugha ya kiengereza, chini ya usimamizi wa profesa Haidari Ghazi Mussawi, mjumbe katika jumuiya ya Al-Ameed, jumla ya mada tano ziliwasilishwa, mada ya kwanza ilikua inasema (Matamshi ya fahari katika khutuba ya Imamu Hassan (a.s) baada ya mkataba wa suluhu) iliwasilishwa na Dokta Zainabu Hussein Alwani kutoka chuo kikuu cha Karbala – kitivo cha elimu ya utalii/ Iraq.

Mada ya pili ilikua inasema: (Maneno ya mantiki kwa mahujaji: khutuba ya Imamu Hassan (a.s) katika mji wa Kufa), iliwasilishwa na Dokta Walidi Ridhwa Hamudi Aljawidi na mkufunzi msaidizi Miyada Hamza Abdulwaahid Hamadi kutoka idara ya malezi Baabil/ Iraq.

Ikafuata mada ya tatu isemayo (Balagha ya kukinzana katika maneno ya Imamu Hassan (a.s)) iliyowasilishwa na mkufunzi Marwah Jabiri Mujiir kutoka Dhiqaar/ Iraq.

Mada ya nne ilikua inasema: (Mpangilio wa turathi za maneno ya Imamu Hassan (a.s)) iliyo wasilishwa na mkufunzi Ali Hussein Abdul-Amiir kutoka idara ya malezi Karbala/ Iraq.

Mada ya tano na ya mwisho ikawa na anuani isemayo (Uchambuzi wa khutuba za Imamu Hassan (a.s) kabla ya kinacho itwa mkataba wa sulhu pamoja na Muawiya), ikawasilishwa na mkufunzi msaidizi Jafari Jaasim Maalih Albadri, kutoka idara ya malezi Dhiqaar
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: