Shamba lenye ukubwa wa dunam 200 la aina tofauti za tende miongoni mwa mashamba ya Saaqi

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanza hatua ya kwanza ya kilimo cha shamba la tende lenye ukubwa wa (dunam 200), ambapo zimepandwa aina adumu za tende, kama vile Barhi na Swa’qi.

Rais wa kitengo Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mradi wa mashamba ya Saaqi unatekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa (dunam 10,250), limetengwa eneo la (dunam 1000) kwa ajili ya kupanda aina adimu za tende hapa Iraq, zenye kupamba vizuri na zinazo endana na mazingira ya jangwa la Karbala”.

Akaongeza kuwa: “Upandaji wa aina hizo ni sehemu ya mkakati wa kuboresha mradi, hatua hii tumebaini mbegu nadra za tende na ndio tunazopanda”.

Akafafanua kuwa: “Tunapanda kwa kufuata mbinu za kisasa, kuanzia umbali kati ya mche na mche, umwagiliaji wa mateno, tulianza kusawazisha ardhi na kuisamadia, pamoja na kuainisha sehemu ya kupanda kila aina kwa kutumia vifaa vya kisasa, tutaendelea kupanda aina adimu zilizo ainishwa ambazo zitaongeza uzalishaji wa shamba”.

Kumbuka kuwa mradi wa (mashamba ya Saaqi) ni miongoni mwa miradi muhimu inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, umefanikiwa kufikia malengo makuu, ikiwemo kutunza maji ya visima yanayo weza kutumika wakati wowote likitokea tatizo la maji ya kawaida, na ishara za upungufu wa maji zimeanza kuonekana mwaka baada ya mwaka, sambamba na kutumia ardhi hiyo kwa kilimo cha mazao mbalimbali zikiwemo tende.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: