Wataalamu wa Alkafeel wanaotoa huduma za afya wanaendesha mafunzo ya kuokoa majeruhi vitani

Maoni katika picha
Wataalam wa Alkafeel wa uokozi na huduma za afya chini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanaendesha semina ya uokozi vitani kupitia program ya usaidiaji wa majeruhi vitani (TCCC) ambayo ni semina ya hamsini na sita mfululizo.

Semina inahusisha watu kumi na moja kutoka vikosi tofauti na viongozi wa opresheni za (Hashdu-Sha’abi) itaendelea kwa muda wa siku tano kwa kutumia saa kumi za masomo kila siku.

Semina imejikita katika kuwafundisha mbinu za kuokoa majeruhi na kulinda uhai wake katikati ya vita, ikiwa ni pamoja na kuokoa mtu mwenye majeraha makubwa na maumivu ya kifua, kuvunjika mifupa na tatizo la hewa.

Wanafundishwa mada nyingi, miongoni mwake ni: kuamiliana na mazingira magumu, majeraha ya kifuani, majeraha makubwa na madogo, aina zote za uvunjikaji wa mifupa.

Tambua kuwa wanafundishwa kwa nadhariyya kwa kiasi cha asilimia %30 na kwa vitendo asilimia %70, kwa kufuata taratibu za kimataifa, kila hatua wanapewa majaribio kupima uwezo wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: