Waziri wa elimu ya juu na tafiti za kielimu atoa shukrani na pongezi kwa chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Waziri wa elimu ya juu Dokta Nabiil Kaadhim Abdu Swahibu, wametoa shukrani na pongezi kwa chuo kikuu cha Alkafeel, kutokana na juhudu kubwa zinazo fanywa na chuo hicho kuhakikisha kinafikia malengo yake ya kutoa elimu bora.

Dokta Nabiil Kaadhim akapongeza kazi ya pekee iliyofanywa na chuo ya kuondoa changamoto za wanafunzi wakati wa mitihani ya mwisho wa mwaka (2020 – 2021), sambamba na kuweka mazingira ya chuo katika hali nzuri, akawatakia mafanikio mema na kuendelea kutumikia raia wa Iraq.

Kumbuka kuwa Chuo kikuu cha Alkafeel katika mji wa Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinafanya kila kiwezolo ili kuboresha huduma zake katika sekta ya elimu, utamaduni, malezi na tafiti za kielimu hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: