Ataba mbili tukufu zinafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Marjaa Dini mkuu Sayyid Muhammad Saidi Alhakiim (q.s)

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Alasiri ya Jumamosi zimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Udhuma Sayyid Muhammad Saidi Alhakiim (q.s).

Majlisi imefanywa ndani ya uwanja wa katikati ya haram mbili na kuhudhuriwa na kundi kubwa la waumini na viongozi wa Ataba mbili Huseiniyya na Abbasiyya.

Marjaa Dini mkuu Sayyid Alhakiim (q.s) alifariki kwa maradhi ya moyo siku ya Ijumaa iliyopita (25 Muharam 2443h) sawa na tarehe (3 Septemba 2021m), umati mkubwa wa watu ulijitokeza kushindikiza jeneza lake katika mji wa Karbala na Najafu.

Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani alituma salam za rambirambi kwenye hauza za kielimu kwa kumpoteza mtu muhimu na faqihi mkubwa kufuatia kifo cha Ayatullahi Sayyid Alhakiim (q.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: