Maqaam ya kichwa cha Imamu Hussein (a.s) katika mji wa Naswibiin ina kisa gani?

Maoni katika picha
Msafara wa mateka kutoka familia ya Mtume (s.a.w.w) pamoja na kichwa cha Imamu Hussein (a.s), walipitia sehemu nyingi, kuanzia walipo ondoka Kufa hadi kuwasiri Sham, sehemu mbalimbali walizo simama zimejengwa Maqaam (makumbusho), bila shaka sehemu hizo hazikuzikwa kichwa cha Imamu Hussein (a.s), lakini kiliwekwa au kuhifadhiwa kwa muda fulani, ikiwemo Maqaam tukufu ya Naswibiin.

“Naswibiin” muundo wa neno hilo kwa kiarabu unamaana ya wingi, ni mji wenye kukusanya vitongoji vya visiwa, ni eneo la kuanzia Mosul hadi Sham, kama inavyo semwa kwenye eneo hilo kuna bustani elfu arubaini, kati yake na Sanjaar kuna farsakh tisa, kutoka hapo hadi Mosul ni mwendo wa siku sita, eneo hilo kwa sasa lipo Uturiki mpakani na Sirya, limepakana na mji wa Qamashili wa Sirya.

Baadhi ya vitabu vimeandika kuwa msafara wa mateka ulipo wasili katika mji wa Naswibiin, kiongozi wa mji huo aliamuru upambwe, wakaupamba kwa kuweka zaidi ya vioo elfu moja, na wakapandisha zaidi ya bendera elfu moja kama ishara ya kupokea kichwa cha Imamu Hussein (a.s) na mateka wake, maluuni aliyekua amebeba kichwa cha Imamu Hussein (a.s) akataka asiingie katika mji huo, farasi wake hakumtii na farasi wengine wote wakagoma hadi wakaingia kwenye mji huo.

Walipo ingia katika mji huo kichwa kikadondoka kutoka juu ya mkuki, mmoja wa walioshuhudia akajua kuwa hicho ndio kichwa cha Imamu Hussein (a.s), akawalaumu na kuwakemea kwa dhambi hiyo, watu wa Sham wakamuua, kisha wakaweka kichwa cha Imamu nje ya mji.. Shekh Abbasi Qummi (q.s) anasema: sehemu kilipo anguka kichwa kitukufu pamejengwa Maqaam (Makumbusho).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: