Basra yaitikia wito wa Arubaini

Maoni katika picha
Watu wa Basra tangu zaidi ya siku tano zilizopita wanajitokeza katika matembezi ya kuelekea Karbala kufanya zaiara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), huku wakipata huduma kubwa kutoka kwa mawakibu za kutoa huduma na vikundi vya Husseiniyya, ulinzi umeimarishwa na vikosi vya ulinzi na usalama, pamoja na kuzingatiwa kanuni za afya kama zilivyo elekezwa na idara ya afya hapa mkoani.

Kwa mujibu wa ripota wa mtandao wa Alkafeel ambaye yupo katika matembezi hayo amesema: Idadi ya mazuwaru inaongezeka kidogokidogo na itafikia kilele cha wingi wake siku mbili zijazo, ambapo asilimia kubwa watakua wanaelekea katika mkoa wa Dhiqaar, na wengine katika mkoa wa Misaan, mikoa ambayo imejiandaa kupokea mazuwaru huao, mazuwaru wanatumia njia tofauti, baadhi yao wanatumia njia kuu na wengine njia ndogo.

Njia zote wanazo tumia kuna mawakibu za kutoa huduma zilizo jiandaa kuhudumia misafara ya mazuwaru hao, kwa kuwapa chakula, vinywaji na malazi, sambamba na huduma za afya na zinginezo. kamera inawaletea baadhi ya picha za matembezi hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: