Idara ya Qur’ani inaendesha shindano la (Fajrul-Hussein)

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kufanya shindano kwa njia ya mtandao chini ya anuani isemayo: (Fajrul-Hussein a.s), la kuhifadhi sutat Fajri kwa mabinti wenye umri wa miaka (7) hadi (12).

Tutaanza kupokea visomo vya washiriki tarehe (15 Safar) hadi tarehe (20 Safar) sawa na tarehe (23 Septemba 2021) hadi tarehe (28 Septemba 2021m).

Washiriki wanatakiwa kutuma rekodi zao za video zisizozidi muda wa dakika mbili kwenye mtandao wa telegram ya idara ya Qur’ani.

Watakaesoma kwa usahihi na kufuata hukumu za usomaji wanaweza kushinda, ikumbukwe kuwa tumeandaa zawadi za washindi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia facebook.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: